Hebrews 7:18-23

18 aKwa upande mmoja, ile amri ya mwanzo isiyofaa na dhaifu imebatilishwa 19 b(kwa maana sheria haikufanya kitu chochote kuwa kikamilifu). Kwa upande mwingine, tumeletewa tumaini lililo bora zaidi ambalo linatuleta karibu na Mungu.

20Nalo tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wengine walikuwa makuhani pasipo kiapo chochote, 21 clakini Isa alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alimwambia: Bwana ameapa
naye hatabadilisha mawazo yake:
‘Wewe ni kuhani milele.’ ”

22 dKwa ajili ya kiapo hiki, Isa amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.

23Basi pamekuwepo na makuhani wengi wa aina hiyo, kwa kuwa kifo kiliwazuia kuendelea na huduma yao ya ukuhani.
Copyright information for SwhKC